Thursday, May 24, 2018

MUME ACHINJA MKE NA MTOTO WIVU WA MAPENZI MKE KUCHEPUKA NA SHEMEJI

  Malunde       Thursday, May 24, 2018

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Omari Matonya anatafutwa na jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kuwaua kwa kuwachinja mke wake na mtoto wao, kisha kukimbia.

Akizungumza na www.eatv.tv, kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Wilbroad Mutafungwa amesema kwamba mtu huyo amefanya tukio hilo nyakati za usiku wakati wakiwa wamelala, huku chanzo kikubwa kikitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

“Mwanamke ambaye anaitwa Moshi Daudi mwenye miaka 24 akiwa na mtoto wake wa mwaka mmoja anayeitwa Omari Matonya, waliuawa kwa kuchinjwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mwanaume anaitwa Omari Matonya mwenye miaka 25, ambaye ni mume wa huyo mama na baba mzazi wa huyo mtoto, baada ya kufanya tukio hilo alitoweka.

 Alifanya tukio hilo wakati familia yake ikiwa imelala na chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi, ambapo huyo marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa na mahusiano na shemeji yake, ambaye ni ndugu yake huyo Matonya anayeitwa Lazima Matonya”, amesema Kamanda Mutafungwa.

Kamanda Mutafungwa amesema mpaka sasa hajapata taarfa zake zozote na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta, ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Chanzo- EATV
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post