KOCHA MPYA WA YANGA KUJA NA MBINU MPYA


Kocha mpya wa Yan­ga mzaliwa wa DR Con­go, Zahera Mwinyi, baada ya kufanya tathmini dhidi ya Simba amewaahidi mashabiki kwamba ana­kuja na mbinu mbadala ili kikosi chake ili kisifungwe tena kirahisi.


Jumapili iliyopita, Yanga ilifungwa bao 1-0 na Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, timu hizo zitakutana tena msimu ujao kwani awali walitoka sare ya bao 1-1 katika ligi hiyo.


Mwinyi aliyeletwa Yanga kuchukua nafasi ya Ko­cha George Lwandamina aliyejiunga na Zesco United ya kwao Zambia, Jumapili iliyopita aliushuhusia mchezo huo akiwa jukwaani kwani hakua na vibali vya kufanya kazi nchini.

Mwinyi alisema ; “Nafurahi kuona mchezo wa Simba dhidi ya timu yangu ya Yanga, limekuwa ni jambo zuri sana kwangu kwani limenipa changamoto kubwa na limenifanya kuwajua mapema wapinzani wangu hasa nitakapoanza kufundi­sha rasmi.”


“Yanga ina wachezaji wa­zuri sana sema kuna mambo machache tu ambayo nitakapoyafanyia kazi kikosi changu kitakuwa imara zaidi kisichofungika kirahisi kwani siyo kibaya kama ambavyo nilikuwa nikiambiwa.

“Kikosi kingekuwa kibaya kwa mchezo ule wa Jumapili tungefungwa mabao mengi sana ila kwa kuwa wapo safi utaona walipambana vya kutosha na hata lile bao ya­likuwa na makosa kidogo tu ya uwanjani,” alisema Mwinyi ambaye amewahi kufundisha Ubelgiji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527