ALIYECHUNGUZA MALI ZA CCM AMRITHI KINANA UKATIBU MKUU CCM...VIONGOZI WENGINE HAWA HAPA


Mwenyekiti wa CCM,Dkt, John Pombe Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu mpya wa CCM Dk. Bashiru Ali 
Katibu Mkuu mpya wa CCM Dk. Bashiru Ali akipongezwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamedi baada ya jina lake kupendekezwa na kisha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM kulipitisha kwa kauli moja, katika kikao cha NEC kwenye ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam, leo Jumanne Mei 29,2018. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli
Dk. Bashiru akiwa ameketi meza kuu baada ya uteuzi.
Dk. Bashiru akizungumza baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM kwenye kikao cha NEC.
Dk. Magufuli akishauriana jambo na Dk. Shein wakati wa kikao hicho
Wajumbe wakishangilia baada ya kumpitisha rasmi Dk. Bashiru kuwa Katibu Mkuu wa CCM
***
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Dk Bashiru Ali kuwa katibu mkuu wa chama hicho.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Mei 29,2018 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema Dk Bashiru ambaye ni mhadhiri wa masuala ya Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ndiye mrithi wa Abdulrahman Kinana aliyestaafu jana.

Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli aliridhia ombi la Kinana kujiuzulu jana.

Dk Bashiru ndiye aliongoza tume ya kuchunguza mali za CCM.

Taarifa ya CCM imesema, Raymond Mangwala ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) na Queen Mlozi, kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT).

Erasto Sima ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post