Monday, May 14, 2018

Picha : DC MUSOMA AZINDUA RASMI SHINDANO LA MISS MARA 2018

  Malunde       Monday, May 14, 2018
Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano amezindua rasmi Shindano la kumtafuta mrembo wa mkoa wa Mara " Miss Mara 2018" linalotarajiwa kufanyika Julai 7,2018.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa shindano hilo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Le Grand Hotel mjini Musoma,Naano amesema kampuni ya Space 2000 Co. Ltd inayoandaa mashindano hayo itafanikiwa kurudisha hadhi ya mashindano hayo ikiwa itafanikiwa kumpata mrembo anayekidhi vigezo na atakayepatikana kwa haki bila kufanya shindano la ubabaishaji na kumpanga mshindi.

Amesema yupo tayari kuwaunga mkono waandaji wa shindano hilo na kuwaunganisha a wadau mbalimbali kwa kuwa hana wasiwasi na waandaaji katika masuala ya burudani na kuwataka kuzunguka mkoa wote wa Mara kwenye wilaya zake kusaka washiriki wa shindano hilo. 

Naye Mkurugenzi Mwenza wa kampuni ya Space 2000 Co Ltd, Abubakar Nyamakato, kampuni yao ina uzoefu wa masuala ya burudani kuahidi kurejesha hadhi ya shindano hilo kama ambavyo walivyoaminiwa na kampuni ya Look chini ya Basira Mwanukuzi ambao ndiyo waandaaji wapya wa Shindano la Miss Tanzania.

Nyamakato amesema kutokana na kuaminiwa na kampuni ya Look katika kuandaa shindano hilo mwaka huu,wamekusudia kufanya shindano la mfano na watazingatia vigezo vyote ambavyo vinahitajika.

Amesema moja ya malengo ambayo mshindi wa miss Mara atakayepatikana ni kuhakikisha anakuwa balozi mzuri wa kuuwakilisha mkoa wa Mara hususani katika masuala ya utalii wa ndani kutokana na rasilimali zilizopo na kupingana na masuala ya ukeketaji,mimba na ndoa za utotoni.
Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Shindano la kumtafuta mrembo wa mkoa wa Mara " Miss Mara 2018" 
Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano akizindua  Shindano la kumtafuta mrembo wa mkoa wa Mara " Miss Mara 2018" 

Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo
Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Space, Dj Timba (kulia) akiwa na mfanyabiashara wa nguo mjini Musoma maarufu kwa jina Chalz Colection
Meneja wa kampuni ya Space- Big Hassan akiwa ametulia kwenye uzinduzi huo 
MC Kiokote akiendesha uzinduzi huo huku juu wadau mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo
Mkurugenzi Abuu akizungumza kwenye uzinduzi huo 
Mkuu wa kitengo cha matangazo Miss Mara 2018, Shomari Binda akitoa maelezo kuhusiana na shindano hilo.
Mkuu wa wilaya akizungumza kwenye uzinduzi huo 
Wadada wa kampuni ya Space wakipata vitafunnwa
Mkuu wa wilaya akiwa na wakurugenzi wa kampuni ya Space ambao ndiyo waandaaji 
Baadhi ya wadau waliofika kwenye uzinduzi huo 
Wafanyakazi wa kampuni ya Space wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi 
Warembo wakijiandaa kula soseji

Warembo wakipiga selfie
Mkurugenzi Abuu na wadau
Wadau wakibadilishana mawazo 

PICHA ZOTE NA SHOMARI BINDA
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post