Wednesday, May 2, 2018

AJIRA 10,140 ZA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI KUTOLEWA JUNI

  Malunde       Wednesday, May 2, 2018
Serikali imesema Juni 30, 2018 inatarajia kutoa ajira 10,140 za walimu wa shule za msingi nchini.

Hayo yamesemwa leo Mei 2, 2018 Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Ludewa (CCM), Deogratius Ngalawa.

Katika swali lake, Ngalawa alitaka kupata majibu ya Serikali kuhusu upungufu wa walimu 500 wa shule za msingi na jinsi litavyoshughulikiwa.

Akijibu swali hilo, Kakunda amesema; "Tunaendelea na mchakato kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Taifa kwa kupitia vyeti vya vya walimu na tunategemea ifikapo Juni 30 kuwaajiri."
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post