WASAFI TV IMEANZA KURUSHA MATANGAZO LEO APRILI 2,2018

Kituo kipya cha runinga cha Wasafi TV leo Aprili 02, 2018 kimeanza kurusha matangazo yake mubashara kupitia ving’amuzi mbalimbali kikiwemo cha Azam TV.


Akithibitisha taarifa hizo, Diamond Platnumz ambaye ndiye mmiliki na muanzilishi wa kituo hicho, amesema kuwa matangazo hayo yameanza kuonekana kuanzia leo na kwa watumiaji wa king’amuzi cha Azam, Wasafi TV itapatikana namba 122 .


Hata hivyo, bado haijajulikana kama Wasafi TV itapatikana kwenye ving’amuzi vingine zaidi ya Azam TV.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527