WACHEZAJI WA YANGA KUPEWA KIFUTA JASHO


Uongozi wa Yanga kupitia Katibu Mkuu wa klabu, Charles Boniface Mkwasa, umetangaza kuwa utawapa kifuta jasho wachezaji wake baada ya kuiwezesha timu kuingia hatua ya makundi.
Yanga wamefikia hatua hiyo ili kuzidi kutoa hamasa kwa wacheza ambao wamesaidia kikosi hicho kuiondosha Wolaita Dicha SC kutoka Ethiopia.
Mkwasa ameeleza kuwa watafanya hivyo ikiwa ni sehemu ya kutia morali kwa wachezaji baada ya kazi nzito katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Tayari kikosi kwa ujumla kimesharejea nchini na sasa kitakuwa tayari kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City FC.
Yanga imesonga mbele mpaka hatua ya makundi ya mashindano hayo kufuatia kuiondoa Dicha kwa idadi ya mabao 2-1.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.