RAIS MAGUFULI AMTUMBUA MKURUGENZI WA MPWAPWA.ANACHUNGUZWA

Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mohamed Maje kuanzia leo kwa kilichoelezwa kushindwa kutimiza majukumu yake.


Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Tamisemi Mussa Iyombe inasema Maje amesababishia hasara serikali ikiwamo kushindwa hata kukusanya mapato ya serikali.


"Hata makusanyo ya mwaka huu hatujui anapeleka wapi hadi leo amekusanya asilimia 24 tu katika halmashari ya Kongwa na Mpwapwa licha ya kuwa na vyanzo vingi vya mapato.


Iyombe amesema Mkurugenzi huyo kwa sasa yupo chini ya uchunguzi.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.