RAIS MAGUFULI AMTEUA DK. MAFUMIKO KUWA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

Rais John Magufuli amemteua Dk Fidelice Mafumiko kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.


Uteuzi huo wa Dk Mafumiko umeanza Jumanne Aprili 3, 2018.


Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Dk Mafumiko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).


Dk Mafumiko anachukua nafasi ya Profesa Samuel Manyele ambaye amemaliza muda wake.

Theme images by rion819. Powered by Blogger.