Thursday, April 5, 2018

Picha & Video : MAMA USHAURI AANGUSHA BURUDANI BABU KUBWA KISHAPU....NGOMA YA MAGUFULI YAMCHANGANYA RC

  Malunde       Thursday, April 5, 2018
Msanii wa nyimbo za asili Mama Ushauri maarufu Full Melody Classic kutoka Tinde - Shinyanga leo Alhamis Aprili 5,2018 ametoa burudani babu kubwa kwa maelfu ya wananchi waliohudhuria Kilele cha maadhimisho ya upandaji miti kitaifa yaliyofanyika wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
 

Maadhimisho hayo yamefanyika katika uwanja wa SHIRECU Mji wa Mhunze wilayani Kishapu ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk, Hamis Kigwangala.

Katika sherehe hizo za upandaji miti,Mama Ushauri alitumia nafasi hiyo kuwahamisha wananchi kupanda miti kupitia wimbo wake maalumu aliotunga kuelimisha kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti.

Pamoja na wimbo huo,Mama Ushauri pia alicheza nyimbo kadhaa ukiwemo unaomhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambao ulimvutia mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na kuingia uwanjani kucheza.

Malunde1 blog imekusogezea Uhondo wote…Mwandishi wetu Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio ametuletea video na picha wakati Mama Ushauri akidondosha burudani.

Mama Ushauri wimbo maalum upandaji miti

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akicheza wimbo wa Magufuli kutoka kwa MamaUshauri 

Vijana wa Sarakasi wa Mama Ushauri wakitoa burudani

Sekunde 24 Mama Ushauri na madensa wake wakikata viuno balaa!

TAZAMA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Msanii wa nyimbo za asili Mama Ushauri maarufu Full Melody Classic kutoka Tinde wilaya ya Shinyanga akicheza na madensa/ wanenguaji wake wakati akiimba wimbo unaohamasisha wananchi kupanda miti kwenye kilele cha maadhimisho ya upandaji miti kitaifa wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.
Mama Ushauri akiimba wimbo kuhusu upandaji miti
Mama Ushauri akiendelea kutoa burudani
Mama Ushauri akiimba wimbo kuhusu Rais Magufuli na CCM (Tazama video live ipo hapo juu)
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack akicheza wimbo wa Rais Magufuli (Tazama video hapo juu)
Mambo ni motooo!! Ngoma ya Magufuli na CCM imemkolea Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu,mheshimiwa Nyabaganga Talaba naye akiserebuka.
Mama Ushauri akiimba huku madensa wakicheza
Mama Ushauri akiimba wimbo wa Mama ni Mama unaomhusu mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hamad Hilal
Burudani inaendelea...
Madensa/wanenguaji wa Mama Ushauri wakicheza wimbo wa "Baba Jeni"
Madensa/wanenguaji wa Mama Ushauri wakicheza kwa madoido
Burudani inaendelea
Hatari lakini salama!!! Vijana wa sarakasi wa Mama Ushauri wakionesha vipaji vyao...
Kijana wa sarakasi akifanya yake..
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangala akifuatilia burudani
Mkuu wa wilaya ya Kishapu,mheshimiwa Nyabaganga Talaba (katikati) akimwambia jambo mkuu wa mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Zainab Telack 
Viongozi wa dini,taasisi na siasa wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea..


Mama ushauri akiendelea kutoa burudani
Vijana wakicheza..
Madensa/wanenguaji wakifanya yao.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post