MWANAMKE ALIYENYONYESHA TEMBO 230 AFARIKI DUNIA

Kutoka nchini Kenya Mhifadhi wa Tembo Daphne Sheldrick amefariki dunia kwa maradhi ya saratani akiwa na umri wa miaka 83, jana April 13, 2018.

Alisaidia kuokoa maisha ya tembo zaidi ya 230 wengi wao ambao walipoteza mama zao kwa ujangili au ukame kwa kutengeneza mpango maalumu wa kuwapatia maziwa na kufanikiwa kwa ufanisi.

Daphne alizaliwa na kukulia nchini Kenya, alitumia takribani nusu ya miaka yake ya kwanza kazini, akifanya kazi pamoja na mume wake ambaye alikuwa Mwingereza David, ambaye ndiye aliyegundua Hifadhi ya Taifa Tsavo Mashariki nchini Kenya.

Baada ya kifo cha mumewe mwaka wa 1977, alianzisha mfuko wa David Sheldrick Wildlife Trust (DSWT), ambao unajulikana zaidi kwa kuokoa na kuimarisha tembo yatima porini.

Ilimchukua miaka yake 28 kufanikiwa kutengeneza formula maalum ya kunyonyesha tembo kwa maziwa ya chupa.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527