MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE APIGWA NA WALIMU HADI KULAZWA HOSPITALINB- Picha haihusiani na habari hapa chini
Waalimu watatu wa Shule ya Msingi Kimamba B iliyopo Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wanadaiwa kumpiga mwanafunzi wa darasa la 4 mwenye umri wa miaka 10 na kumsababishia kulazwa katika taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI) Jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa mama wa mtoto huyo, Bi. Phily Muhebi mkazi wa Kilosa amesema kuwa mwanaye alijeruhiwa vibaya kwa kipigo kutoka kwa waalimu hao Machi 19, mwaka huu kwa kosa aliloelezwa na wanafunzi wenzake kuwa ni baada ya mwenzake mmoja kulalamika kwa walimu kuwa amempaka upupu.

Taarifa za kujeruhiwa kwa mtoto huyo zimefikishwa Polisi huku Mama huyu akilalamikia vitisho alivyopewa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo licha ya mwanaye kuumizwa vibaya na walimu wake.

Mama wa Mtoto huyo amesema kwa sasa anahangaikia matibabu ya mwanaye huyo huku akihofia uwezo wake wa kumudu gharama za matibabu, ambapo ameiomba Wizara ya Elimu kuingilia kati suala hilo sambamba na kuwezesha upatikanaji wa haki dhidi ya unyama aliofanyiwa mwanaye.

Uchunguzi wa Afya mtoto huyo unaendelea, huku taasisi ya mifupa MOI ikiiahidi kutoa tarifa kamili punde baada ya uchunguzi wa kina wa kitabibu wanaoufanya utakapokamilika.
Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post