MTOTO MKUBWA WA LOWASSA AMSHANGAA MWANAMKE ANAYEDAI LOWASSA KAMTELEKEZA

Lowassa na binti huyo
Fred Lowassa

Mtoto mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Fred Lowassa, ameshangaa mwanamke aliyejitokeza na kudai kuwa ni binti wa mwanasiasa huyo.


Aidha, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutumia vizuri mamlaka yake.

Kauli hiyo ya Fred imekuja baada ya mwanamke mmoja mkazi wa Kigamboni, Fatuma Lowassa (31), kujitokeza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, jana Jumanne Aprili 10, akidai kutelekezwa na baba yake ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.

Akiwa Monduli mkoani Arusha, Fred ametoa tamko akisema; “Nimesikia mwanamama mmoja akiongea kuwa yeye ni ndugu yetu kule Dar es Salaam.

“Kwa taarifa tu sisi watu wa Monduli kwetu watoto ni baraka na neema, nimeshangaa ametukosa ukoo mzima kujitambulisha.

“Namwambia Paul Makonda, nimetoka naye mbali sana, nasikitika sana anavyotumia nafasi yake vibaya kwa manufaa anayoyajua. Makonda nimekulea.” Ameandika Fred.

Mwanamke huyo amejitokeza jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ikiwa ni mwendelezo wa Makonda kuonana na wanawake waliotelekezwa na watoto na waume zao.

Mwanamke huyo amesema yuko tayari kupima kipimo cha DNA na Lowasa kuthibitisha kama kweli ni baba yake huku akijinasibu kumtafuta baba yake huyo kwa muda mrefu bila mafanikio.

“Nilipeleka barua Ikulu kuomba kuonana na baba kipindi akiwa Waziri Mkuu lakini niliitwa mimi na mama katika Klabu ya Mamba iliyopo Kinondoni, alikuja mwanamume akiwa kwenye gari lenye ‘tinted’ akatuhoji mimi na mama akaondoka hakutupa majibu yoyote hadi leo,” amesema Fatuma.

Aidha, amesema aliwahi kukutana na Fred na akamuahidi kumsaidia lakini hadi sasa amekuwa kimya.

==>Msikilize Hapo Chini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527