Friday, April 13, 2018

MCHUNGAJI MSIGWA AMCHANA KITILA MKUMBO KUKAZANA NA MAASKOFU

  Malunde       Friday, April 13, 2018
Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kumchana Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo na kusema kuwa anashindwa kutafuta namna ya kuwatua wamama ndoo kichwani amekazana kuandika barua za kuwajibu maaskofu.

Msigwa amesema hayo bungeni na kudai kuwa serikali imekuwa ikipandisha watu vyeo na kuwapa nafasi watu wengine ambao hawaendi kuleta tija katika nafasi hizo kutokana na kukosa uzoefu wa kazi au kukosa uelewa wa mambo, jambo ambalo amedai limepelekea halmashauri nyingi kufanya vibaya. 

"Kwenye taifa letu kunapofanyika promotion au appointment au replacement kwenye eneo lolote haitegemeani na merits, unapomchagua Katibu Mkuu wa wizara unamchagua kwa vigezo gani unataka akaongeze thamani gani, unapomchagua Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya unawachagua kwa vigezo gani, tulilalamika wakati serikali hii inaingia madarakani kwamba mmewatoa wakurugenzi waliokuwa wazuri waliokuwa wanafanya kazi kwa waledi katika ofisi zao lakini wakaletwa watu tu kwa sababu wanavaa sare za CCM na leo tumeona jinsi ambavyo halmshauri zetu zinavyoshindwa kufanya kazi, kumekuwa na ubaguzi wa hali ya juu sana na upendeleo kwa sababu hawa wote walioteuliwa hawaendani na kazi walizopewa" alisema Msigwa 

Mchungaji Msigwa aliendelea kutolea ufafanuzi hilo kwa kumtolea mfano Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo 

"Kwa mfano ofisi ya Katibu Mkuu ni ofisi serious kabisa unamuona mtu kama Prof. Kitila Mkumbo badala ya kushughulika na namna ya kumtua mama ndoo kichwani yeye amekazana anaandika kuwajibu maaskofu ambao wanashughulika na roho za watu mtaani, badala ya kukaa kwenye ofisi, haya ndiyo tunayosema mtu hajui anaenda kuongeza thamani gani na nimezungumza mambo ya replacement haya unamchukua mtu kama Kitila anazungumzia mambo ya elimu unampeleka kwenye mambo ya maji anakaa ofisini badala ya kuzungumza mambo ya kumtua mama ndoo kichwani ambalo ni wazo zuri yeye anakazana anaandika anataka kumjibu askofu kwa sababu ya mawazo aliyotoa kwamba hakuna demokrasia nchi hii" alisisitiza Msigwa
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post