Monday, April 16, 2018

MAMLAKA YA HALI HEWA - TMA YATOA TAHADHARI MPYA...MVUA KUBWA KUNYESHA

  Malunde       Monday, April 16, 2018
Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa vipindi vya mvua kubwa na upepo mkali unaozidi km 40 kwa saa katika maeneo yote ya Pwani kuanzia saa 24 zijazo kutoka sasa.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo (Jumatatu) na kudai kutakuwepo vipindi vya mvua kubwa katika saa 24 ambavyo vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Morogoro, Dar es Salaam, Pwani, Tanga Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mbali na hilo, TMA imesema kuna tarajiwa vipindi vifupi vya mvua kubwa vinavyotarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Mara, Simiyu, Kigoma, Dodoma, Singida, Kilimanjaro, Arusha na Manyara huku upepo wa pwani unatarajiwa kuvuma kutoka kusini kwa kasi ya km 40 kwa saa kwa Pwani yote.

Kwa taarifa kamili angalia hapa chini..

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post