Tuesday, April 17, 2018

DIAMOND AKAMATWA NA POLISI KWA KUSAMBAZA PICHA CHAFU MTANDAONI...WAZIRI MWAKYEMBE APONDA

  Malunde       Tuesday, April 17, 2018
Waziri wa Habari, Harrison Mwakyembe, amesema msanii Diamond Platnumz alikamatwa jana kwa makosa ya kusambaza picha zilizokosa maadili mitandaoni na sasa anahojiwa na polisi.


Akizungumza bungeni leo Aprili 17, Waziri Mwakyembe amesema serikali imeshatunga sheria inayowabana wasanii na kudhibiti maudhui yasiyo na maadili mitandaoni.


Mbali na hilo Mwakyembe ameagiza msanii mwingine Nandi kusakwa na polisi akisisitiza kauli yake kuwa Tanzania siyo kokoro la uchafu.


Ametoa kauli hiyo wakati anajibu swali la nyongeza la mbunge wa Ulanga Godluck Mlinga aliyetaka kujua serikali ina mkakati gani kukomesha tabia za baadhi ya watu wanaotumia mitandao vibaya ikiwemo kuhamasisha masuala ya ushoga.


Awali serikali ilitaja changamoto kubwa inayolikabili taifa ni athari ya utamaduni wa nje katika maadili, mila na desturi za Mtanzania kutokana na kuwepo na muingiliano mkubwa wa watu duniani.


Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Juliana Shonza wakati akijibu swali la mbunge, Nuru Awadh Bafadhili.


Mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mkakati gani madhubuti wa kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanasimamia maadili.


Hata hivyo Shonza amesema kinacholeta shida hadi nyimbo kuwa hazina maadili ni tabia ya wasanii kutopeleka nyimbo zao kuhaririwa katika baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post