AUNTY EZEKIEL AWATAKA WASANII WA BONGO MOVIE WAACHE KUMLILIA KANUMBA

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka na kuwaasa wasanii wenzake wa Bongo movie waache kumlilia msanii mwenzao Steven Kanumba na badala yake waenzi kazi zake.


Steven Kanumba alikuwa msanii wa Bongo movie ambaye alikuwa ni mfano wa kuigwa na kila msanii kwani uwezo wake wa kuigiza na ubunifu uliweza kwa kiasi kikubwa kuifikisha tasnia hiyo mbali.


Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu tasnia hii ikumbuke siku ya kifo chake ambayo inaitwa Kanumba Day, Aunty Ezekiel amefunguka na kusema sasa kuomboleza kifo chake tu kumetosha.


Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Ijumaa, Aunty Ezekiel amesema kuwa mara nyingi wasanii wanapoadhimisha kumbukumbu ya kifo chake, wanakuwa wanalia au wengine wanasononeka mara kwa mara hiyo inakuwa inazidi kurudisha tasnia nyuma badala yake wasanii wakaze buti waweze kufika alipokuwa amefika yeye.


"Najua wazi uchungu upo lakini inabidi tuache sasa kulia badala yake tujitahidi kufikia pale alipotuacha ili tuzidi kusonga mbele maana tukisema kulia kila siku hatuwezi kufika tunapotaka hata siku moja”.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527