ABDUL NONDO APEWA TUZO YA MTETEZI CHIPUKIZI WA HAKI ZA BINADAMU

Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Omar Nondo amepata tuzo kama mtetezi kijana chipukizi wa haki za binadamu (wanafunzi) Tanzania, tuzo aliyopewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).
Abdul Nondo amesema kuwa tuzo hiyo kwake imekuwa na maana kubwa na kuweza kuinua ari mpya ya kuzidi kuwatetea wanafunzi katika haki zao katika masuala mbalimbali nchini na kudai tuzo hiyo imezidi kumuimarisha zaidi na kutokana tamaa na changamoto mbalimbali anazopitia katika kutetea haki za wanafunzi. 

"Kwanza namshukuru Mwenyezimungu kwa kunipa Afya njema, pia wazazi wangu na viongozi wenzangu wa TSNP na watanzania wote kwa ujumla kwa faraja zao na matumaini yao kwangu. Napenda kutoa shukrani zangu za Dhati kwa Mtandao wa watetezi wa haki Za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kutambua mchango wetu TSNP kwa kunizawadia tuzo kama mtetezi kijana chipukizi wa haki za binadamu (wanafunzi) Tanzania nimefarijika saana" 

Nondo amesema kuwa kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za serikali na taasisi hizo zimekuwa zikipokea na kusikia na kufanyia kazi baadhi ya mambo ambayo wamekuwa wakiyasemea. 

"TSNP pia tumekuwa tukitetea haki za wanafunzi kwa kushirikiana pia na baadhi ya taasisi za kiserikali, wizara ya elimu,wizara ya Tamisemi ,bodi ya mikopo na Tume ya vyuo vikuu zimekuwa zikisikia na kutatua shida za wanafunzi ambazo tumekuwa tukizisemea. Tuzo hii ina maana kubwa kwangu na viongozi wa TSNP. Ina maana kubwa ya kuinua hari mpya ya kusemea na kutetea haki za wanafunzi Tanzania katika maswala mbalimbali. Tuzo hii ina maana kuwa changamoto zipo katika sekta yeyote, ila jambo kubwa ni kuwa mvumilivu, mstahimilivu na kutambua kuwa changamoto haziepukiki katika majukumu haya, na kutokubali changamoto hizi kudhoofisha utetezi wa wanafunzi na kurudi nyuma" alisisitiza Abdul Nondo. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527