Tuesday, March 20, 2018

WAZIRI MKUU AKABIDHI MILIONI 5 KWA MJASIRIAMALI MWENYE ULEMAVU WA MIGUU

  Malunde       Tuesday, March 20, 2018
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi Bibi Tecla Hamidu ambaye ni mlemavu wa miguu sh. milioni tano ili aweze kuongezea katika mtaji wake.


Ametoa fedha hizo leo (Jumanne, Machi 20, 2018) ikiwa ni katika kutimiza ahadi yake aliyoitoa Februari 22, 2018 kwenye Mkutano wa Sita wa Wamiliki wa Viwanda na Watumiaji wa simbomilia (barcodes).


Waziri Mkuu alitoa ahadi hiyo baada ya Bibi Tecla ambaye ni mjasiriamali anayejihusisha na ushonaji wa bidhaa mbalimbali zikiwemo nguo kumuomba amchangie sh. 500,000 ili aweze kuongezea mtaji wake.


Wakati akimkabidhi fedha hizo, Waziri Mkuu amesema kwamba anatarajia zitamsaidia katika kuongeza mtaji wake, hivyo atazalisha bidhaa nyingi zenye ubora unaohitajika katika masoko ya ndani na nje.


Kwa upande wake, Bibi Tecla alimshukuru Waziri Mkuu kwa msaada huo na ameahidi kuzitumia fedha hizo kama ilivyo kusudiwa.


“Nashukuru kwa msaada huu kwani kuna watu wanakopa sh. laki mbili ili waongeze mitaji, lakini mimi leo nimepewa milioni tano bure na kiongozi wetu,”


Amesema licha ya kukabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa masoko anaamini tatizo hilo litakuwa historia baada ya kuwa na mtaji wa kutosha kwani atakwenda kuzalisha bidhaa zenye ubora zaidi.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post