VLADIMIR PUTIN ASHINDA TENA URAIS WA URUSI

Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameibuka mshindi kuliongoza taifa hilo kwa muhula mwingine ujao wa miaka sita baada ya kujipatia ushindi mkubwa wa zaidi ya asilimia 76 katika Uchaguzi Mkuu uliomalizika jana Jumapili, Machi 18 nchini humo.


Akizungumza katika mkutano wa kutangazwa mshindi, Putin alisema ushindi wake ni matokeo ya hatua kubwa ya mafanikio aliyoyafikia katika uongozi wake huku akieleza kuwa huo ni uthibitisho wa kukubalika kwa sera zake na kwamba hana mpango wowote wa kufanya marekebisho ya katiba na kusisitiza umoja na mshikamano.


“Hadi hapa sina mpango wowote wa kufanya marekebisho yoyote ya katiba, kuhusiana na unyekiti na serikali kwa ujumla. Nilikwisha sema awali kwamba nafikiria suala hilo. Lakini kuanzia leo naanza kufikiria kwa undani, kwa sababu nilipaswa kusubiria matokeo ya uchaguzi kwanza,” alisema Putin.


Akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari Putin alikwepa swali alilotakiwa kueleza kama atagombea katika muhula ujao pia.


“Kwangu kile mnachotaka kuniuliza inakuwa kama mizaha Fulani hivi, hebu tuhesabu, ina maana nitasalia madarakani hadi nikiwa na miaka 100? Hapana hapana hapana.”


Ushindi huu mkubwa ambao ulitarajiwa, umekuwa na ongezeko la kura ikilinganishwa na ushindi wa asilimia 64 mwaka 2012. Ambapo mpinzani wa karibu wa Putin milionea Pavel Grudinin alipata asimilia 12.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527