KIKWETE : WANAVYOSIFIA TIMU ZAO KWA MATOKEO UNAWEZA SEMA WAMESHINDA...UJINGA MTUPU | MALUNDE 1 BLOG

Monday, March 19, 2018

KIKWETE : WANAVYOSIFIA TIMU ZAO KWA MATOKEO UNAWEZA SEMA WAMESHINDA...UJINGA MTUPU

  Malunde       Monday, March 19, 2018

Baada ya timu za Simba na Yanga kutolewa kweney michuano ya kimataifa ngazi ya vilabu barani Afrika, Mbunge wa Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete amewataka viongozi wa vilabu hivyo kujitathmini.

Mbali na viongozi wa vilabu vya Simba na Yanga, Ridhiwani pia ameoneshwa kushangazwa na mashabiki wa soka nchini kwa namna ambavyo wanazisifu timu hizo kwa kutoa suluhu ugenini na kushindwa kupata matokeo viwanja vya nyumbani.

Yanga imetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Township Rollers ya Botswana baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 jijini Dar es salaam na kisha jumamosi iliyopita kutoa suluhu ugenini hivyo kutupwa nje ya michuano.

Simba wenyewe wameondolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na klabu ya Al Masry ya Misri baada ya kutoa sare ya mabao 2-2 jijini Dar es salaam kabla ya jumamosi usiku kutoa suluhu na kutolewa kwa sheria ya bao la ugenini.

''Magazeti yetu na washabiki wetu wanavyozisifia timu zao kwa matokeo ya Jana unaweza sema wameshinda. UJINGA MTUPU yaani NAWASHANGAA SANA.kwa sifa zipi hizo Suluhu za Ugenini na Kushindwa kutumia Viwanja vya Nyumbani. AIBU KWENU Viongozi wa Mpira.Jipangeni Vizuri Mashindano ni Kushinda'', ameandika.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post