UNICEF YATOA RIPOTI KUHUSU HALI YA NDOA ZA UTOTONI DUNIANI

 Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetoa ripoti inayoeleza kupungua kwa kesi za mimba katika umri mdogo duniani kote.

Shirika hilo limeeleza kuwa takribanI ndoa za utotoni Milioni 25 zimezuiwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ambapo kwa sasa mtoto mmoja kati ya watano wanaolewa kabla ya umri wa miaka 18 ukilinganisha na mmoja kati ya wanne aliyekuwa anaolewa kipindi hicho.

Nchi za kusini mwa Bara la Asia pia zimepunguza ndoa za utotoni huku Afrika ikiendelea pia kujitahidi kukabiliana na tatizo hilo ambapo kwa nchi kama Ethiopia imepunguza tatizo hilo kwa theluthi.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa mzigo wa ndoa za utotoni unaendelea kuzilemea nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambako jitihada zaidi zinahitajika ili kuondoa tatizo hilo kabisa.

UNICEF inasema kuwa mmoja kati ya watoto watatu wanapitia ndoa za utotoni kwa kipindi hiki Afrika ukilinganisha na mmoja kati ya watoto watano waliokuwa wakiolewa miaka kumi iliyopita.

Viongozi wa dunia wameapa kumaliza tatizo la ndoa za utotoni ifikapo mwaka 2030 chini ya Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527