TRUMP AKUBALI KUKUTANA NA KIM JONG UN

Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani ya mwezi Mei mwaka huu,na hivyo kuweka historia kufuatia kutokuwepo rais wa Marekani ambaye amewahi kuonana na kiongozi mkuu wa Korea kaskazini.


Hata hivyo mahala watakapokutana viongozi panasalia kuwa siri kwa sasa,na pia Marekani imesisitiza kuwa pamoja na kukubali ombi hilo la rais Kim Jong Un lakini bado vikwazo vitasalia pale pale.


Tangazo hilo la kwamba rais Trump amekubali kukutana na Kim Jong Un,limetolewa na viongozi wa juu wa Korea Kusini uliofika mjini Washington kuwasilisha barua ya ombi hilo kutoka kwa Korea Kaskazini.


Kim pia amekubali kusitisha mpango wake wa nyuklia na majaribio yake ya makombora,msimamo ambao ni tofauti na aliokuwa nao rais huyo Kim Jong Un.


Hatua hii iliyofikiwa ya rais Kim Jong Un kulegeza msimamo ni matokeo ya mazungumzo mazito yaliyofanywa wiki chache zilizopita ujumbe wa Korea Kusini kukutana na kiongozi huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527