Saturday, March 17, 2018

SIMBA YATUPWA NJE MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA - CAF

  mtilah       Saturday, March 17, 2018
Wekundu wa Msimbazi Simba safari yao ya kuwania kufuzu kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Africa CAF, imehitimishwa leo katika uwanja wa Port Said nchini Misry baada ya kucheza mchezo wao wa marudiano dhidi ya Al Masry.

Simba SC katika mchezo wa kwanza uwanja wa Taifa Dar es Salaam ikiwa nyumbani ilifanya kosa la kuruhusu kufungwa magoli mawili katika mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2, hivyo leo walikuwa wanahitajika kupata walau ushindi wa kuanzia goli 1-0 au sare ya kuanzia 3-3.

Kwa bahati mbaya Simba wameshindwa kupata matokeo ugenini dhidi ya Al Masry na kujikuta wakilazimishwa sare tasa (0-0), hivyo kutokana na mchezo wa kwanza wa nyumbani walitoka sare ya 2-2, wanaondolewa katika michuano hiyo kwa goli la ugenini, hivyo sasa amesalia katika michuano ya Ligi Kuu pekee.

Picha za matukio ya uwanjaniUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post