SIMBA YALAZIMISHWA SARE YA 3 - 3 NA STAND UNITED

Baada ya klabu ya soka ya Simba leo kulazimishwa sare ya mabao 3-3 na Stand United, imekuwa ndio mechi ya kwanza kwa mlinda mlango wa klabu hiyo Aishi Manula kuruhusu mabao mengi kwenye mechi moja.

Simba ambayo ilikuwa ikiwakosa nyota wake washambuliaji Emmanuel Okwi na John Bocco wote kwa pamoja kwa mara ya kwanza imeshuhudiwa ikifunga mabao na kusawazishiwa.

Mabao ya Simba yalifungwa na Asante Kwasi, Laudit Mavugo, Nicolas Gyan huku yale ya Stand United yakifungwa na Tariq Seif, Aroon Lulambo na Blaise Baraye.

Kwa matokeo hayo Simba imesalia kileleni baada ya mechi 20 za ligi msimu huu ikiwa na alama 46 mbele ya Yanga yenye michezo 19 na alama 40 kwenye nafasi ya pili.

Baada ya mchezo huu wa ligi Simba itaingia kambini tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry ya Misri Alhamisi Machi 7.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.