Tuesday, March 6, 2018

SIMBA YAWEKA MIKAKATI YA USHINDI DHIDI YA AL MASRY KESHO

  Malunde       Tuesday, March 6, 2018

Kuelekea mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry benchi la ufundi la Klabu ya Simba limeweka wazi mikakati yake ya kuhakikisha wanaondoka na ushindi kwenye mtanange huo muhimu.

Simba wanatarajia kucheza kesho katika dimba la Uwanja wa Taifa kuanzia saa 12 jioni ukiwa ni mchezo wa pili wa kimataifa baada ya kuwatoa Gendamarie ya Djibout.

Akizungumzia mchezo huo leo jijini Dar es Salaam, Nahodha wa Simba John Raphael Bocco amesema wapo tayari kucheza vizuri na kwa bidii kesho dhidi ya Al Masry ili washinde.

Kocha Mkuu, Mfaransa, Pierre Lechantre amesema baada ya maandalizi mazuri, vijana wake wapo tayari kwa mchezo wa kesho.

Hats hivyo Bocco amesisitiza anafahamu utakuwa mchezo mgumu kwa sababu Al Masry ni timu nzuri kwa rekodi zake na matokeo yake ya nyuma.

Pia Bocco amesema hata Simba ni timu nzuri na iona rekodi nzuri pia kwenye michuano ya Afrika, hivyo mchezo wa kesho utakuwa wa ushindani mkubwa.

Bocco amewaomba wapenzi wa Simba kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa kesho kuishangilia timu yao ili iweze kupata ushindi nyumbani. 

Baada ya mchezo wa kesho, timu hizo zitarudiana siku 10 baadaye mjini Cairo, Misri na mshindi wa jumla ataingia kwenye mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi kwa kucheza na moja ya timu zilizotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu zinazoingia hatua ya makundi Kombe la Shirikisho hupatiwa dola za Kimarekani 150,000 zaidi ya Sh.mlioni 300 ambazo huongezeka kulingana na matokeo zaidi kuanzia hatua hiyo.


Bingwa wa Kombe la Shirikisho hupata Dola za Kimarekani 625,000 zaidi ya Sh. bilioni 1.5, mshindi wa Pili wakati mshindi wa pili wa Kundi hupata dola 239,000 sawa na wa tatu wakati mshindi wa nne hupata dola 150,000.
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post