POLISI MBEYA WAKAMATA VIJANA 29 WANAODAIWA KUWA NI WAUAJI ' WAKOREA WEUSI'


Kundi la vijana 29 wanaodaiwa kufanya uhalifu mkoani Mbeya maarufu kama wakorea weusi wamekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kiuhaulifu, kupiga, kuua na kuibia watu vifaa mbalimbali.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi, Mohammed Mpinga amewaambia wanahabari ofisini kwake leo, Jumamosi kuwa watuhumiwa hao bado wanaendelea kuhojiwa na wengine watafikishwa Mahakamani mara tu baada ya upelelezi utakapokamilika.

Aidha mwanzoni mwa mwezi Januari, 2018, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa nane kutokana na kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambao walifikishwa Mahakamani na kwa sasa wanatumikia vifungo vya nje. 

Kwa upande mwingine, Kamanda Mpinga ametoa wito kwa vijana na jamii kwa ujumla kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wajishughulishe na kazi halali kwa ajili ya kujipati kipato.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.