RAIS ATUHUMIWA KULA FEDHA ZA BENKI


Rais pekee mwanamke Afrika Ameenah Gurib-Fakim wa Mauritius anatarajia kujiuzulu wiki ijayo kufuatia mgogoro wa masuala ya fedha ambapo anatuhumiwa kutumia kadi ya benki iliyotolewa na taasisi ya misaada na kujinufaisha mwenyewe kwa maelfu ya dola.


Ameenah Gurib-Fakim anajiuzulu wiki ijayo baada ya sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa visiwa hivyo.

 Rais Fakim amekanusha kufanya makosa yeyote na kuainisha kwamba amerejesha fedha zilizotamkwa katika sakata hilo.

Rais Gurib-Fakim anafahamika akiwa mwanasayansi na mwaka 2015 aliteuliwa kuwa Rais wa heshima wa taifa hilo Mauritius. Waziri Mkuu Pravind Jugnauth aliwaambia waandishi wa habari kuwa Rais wa Jamhuri ya Mauritius wamekubaliana tarehe atakayo jiuzulu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527