MCHUNGAJI WA KANISA LA KKKT AKAMATWA NA POLISI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limekiri kumhoji Mkuu wa pili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kilimanjaro Kati, Mchungaji Fred Njama.


Hatua ya polisi kumkamata na kumhoji Mchungaji Njama inakuja ikiwa zimepita siku chache tangu kiongozi huyo wa kiroho kutaja mambo sita aliyodai yanaitafuna nchi.


Akizungumza  Machi 17, 2018, Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Hamis Issah amesema; “suala hilo limeshughulikiwa na kamati ya ulinzi ya wilaya na mimi bado halijanifikia ili niwe na nafasi nzuri ya kulizungumzia.”


Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amesema; “suala hilo siwezi kulizungumza katika simu.” Huku akimtaka mwandishi kufika ofisini kwake na atalizungumzia.


Akiwasilisha taarifa yake ya hali ya usharika katika mkutano mkuu wa 21 wa usharika huo wa Kiranga, alitaja mambo hayo kuwa ni kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari, hali ya uchumi kuwa ngumu, miili ya watu kuokotwa, kuminywa kwa vyama vya siasa na ukosefu wa ajira.
Chanzo-Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527