Saturday, March 3, 2018

MBUNGE WA CCM SHINYANGA AMWAGA MABATI KATA YA CHADEMA UJENZI WA ZAHANATI KITANGIRI

  Malunde       Saturday, March 3, 2018
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) ametoa msaada wa mabati 128 kwa ajili ya kuezeka zahanati ya Kitangiri iliyopo katika kata ya Kitangiri manispaa ya Shinyanga ambayo ipo kwenye hatua ya upauaji.

Akizungungumza wakati wa kukabidhi mabati hayo, Mhe. Mayenga juzi alisema uamuzi wa kusaidia hatua hiyo unatokana na ari aliyonayo ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na rais John Pombe Magufuli kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya bila kusafiri umbali mrefu.

"Mheshimiwa diwani wa kata ya Kitangiri wewe ni Chadema lakini nimefarijika umehudhuria zoezi hili la makabidhiano, hii inaonesha dhamira ya kutekeleza ilani yetu ya CCM na unamuunga kwa dhati mheshimiwa rais wetu katika jitihada zake za kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa" alisema Mhe. Mayenga.

Aidha Mayenga alibainisha kuwa maendeleo hayana itikadi za vyama vya siasa,dini wala rangi hivyo kuwaomba wananchi kushirikiana katika kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo itamnufaisha kila mtu.

"Tunataka zahanati hii ikamilike ili wananchi wapate huduma bora za afya,niwakumbushe tu kuwa ugonjwa huwa hauangalii kwamba wewe ni CCM,Chadema au ACT Wazalendo ama chama chochote kile, naomba tuweke pembeni itikadi za vyama kwenye masuala ya maendeleo",aliongeza.
  
Mbunge huyo pia aliahidi kusaidia kununua magodoro yote katika zahanati hiyo pindi itakapokamilika.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Kitangiri Hamis Omar Ngunila (Chadema) alisema amefarijika kwa kata yake kupata msaada huo kwani zahanati hiyo ikikamilika itasaidia kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Kitangiri Mohammed Mulabo (CCM) alisema alilazimika kumuomba mbunge Lucy Mayenga msaada wa mabati kutokana na changamoto ya umbali wa kupata huduma wanayoipata wananchi wake.

Alisema kata hiyo yenye zaidi ya wakazi 13,000 wananchi wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya hivyo wengine kulazimika kwenda zahanati binafsi kupata huduma.

"Mheshimiwa Mayenga leo umetukomboa kwa msaada huu naomba mkurugenzi wa halmashauri amalize haraka hatua zilizobaki ili zahanati ifanye kazi",aliongeza.
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) akizungumza wakati wa kukabidhi mabati 128 kwa ajili ya ujenzi wa zanahati ya Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) akishikana mkono na mwenyekiti wa mtaa wa Kitangiri Mohammed Mulabo (CCM) wakati wa kukabidhi mabati katika zanahati ya Kitangiri. Aliyevaa nguo nyeupe kulia ni diwani wa kata ya Kitangiri Hamis Omar Ngunila (Chadema).
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) akiendelea kukabidhi mabati hayo.
Zoezi la makabidhiano likiendelea
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post