Tuesday, March 20, 2018

MBUNGE SUGU ANAYETUMIKIA KIFUNGO GEREZANI ATOA RAMBIRAMBI KWA DIWANI WA CCM

  Malunde       Tuesday, March 20, 2018
Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Joseph Mbilinyi alimaarufu kama Sugu, Jongwe ametoa rambirambi ya laki moja kwenye msiba wa mama mzazi wa Diwani wa Kata ya Ilemi (CCM) Agatha Ngole. 

Sugu ambaye amefungwa miezi mitano katika gereza la Rwanda Mbeya kwa kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli alipata taarifa akiwa gerezani hapo kuwa diwani huyo amefiwa na mama yake mzazi na kuamua kutoa rambirambi ya shilingi laki moja kwa ajili ya msiba huo. 

Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanatumikia kifungo cha miezi mitano jela katika gereza la Rwanda Mbeya. 

CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini - Nyasa imethibitisha juu ya taarifa hiyo na kusema ni kweli Sugu ametoa rambirambi hiyo kwa diwani huyo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post