Monday, March 12, 2018

MBUNGE AZZA HILAL HAMAD AAHIDI MABATI 100 UJENZI WA BWALO LA CHAKULA SHULE YA TINDE GIRLS

  Malunde       Monday, March 12, 2018

Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad ameahidi kuchangia mabati 100 kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la chakula katika shule ya Sekondari Tinde "Tinde Girls" iliyopo katika kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.

Mheshimiwa Azza alitoa ahadi hiyo Machi 9,2018 wakati wa mahafali ya sita ya kidato cha sita ya shule hiyo alipohudhuria kama mgeni rasmi.

Mbunge huyo alisema elimu bora inategemea uwepo wa mazingira rafiki kwa wananfunzi hivyo kutokana na shule hiyo kutokuwa na bwalo la chakula ambalo litatumika pia kama ukumbi aliahidi kuchangia mabati 100 ili kukamilisha ujenzi huo.

"Shughuli za maendeleo zinahitaji ushirikiano pia wa wananchi badala ya kusubiri serikali pekee,naomba tuchangie ili wanafunzi wetu wawe katika mazingira mazuri,pindi ujenzi utakapoanza nitachangia mabati 100",alisema.

"Pia naahidi kutoa zawadi ya shilingi 500,000/= kwa mwanafunzi atakayefaulu vizuri kwenye masomo ya sayansi,nawasihi wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ili kuendana na sera ya uchumi wa viwanda,pia kataeni kuolewa kabla hamjafikia malengo yenu",alisema mbunge huyo.

Mbunge huyo akishirikiana na mwenyekiti wa bodi ya shule Epaphras Mazina waliendesha harambee kwa ajili ya upanuzi wa shule ikiwemo ujenzi wa bwalo na kufanikiwa kupata fedha taslimu shilingi 266,400/= ahadi ya shilingi 1140,000/=, mabati 109 pamoja na tripu 2 za mawe.

Jumla ya wanafunzi 233 wamehitimu masomo ya kidato cha sita katika shule ya sekondari Tinde "Tinde Girls".
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akicheza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Tinde iliyopo katika kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga wakati wa mahafali ya sita ya kidato cha sita.
Wanafunzi wakiendelea kucheza na Mheshimiwa Azza Hilal Hamad.
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza wakati wa mahafali ya sita ya kidato cha sita shule ya Sekondari Tinde.
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwashukuru wazazi waliojitokeza kumuunga mkono katika harambee ya kuchangia ujenzi wa bwalo la chakula.
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akigawa vyeti
Wanafunzi wa shule ya sekondari Tinde wakitoa burudani
Wazazi wakicheza na wanafunzi
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa katika picha na wanafunzi waliotoa burudani ya maonesho ya mavazi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post