Monday, March 5, 2018

MBOWE AONDOLEWA MASHINE YA KUPUMULIA...AMELAZWA KCMC

  Malunde       Monday, March 5, 2018


Hali ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe aliyelazwa katika Hospitali ya KCMC inaendelea vizuri baada ya kuondolewa mashine ya Oskijeni.

Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene amethibitisha hivyo ambapo amesema kwa sasa anapumua mwenyewe bila msaada wa mashine hiyo.

Mbowe alifikishwa katika hosptali hiyo akiambatana na baadhi ya makada wa chama hicho ya saa 10:30 Jioni jana Jumapili Machi 4, akiwa katika hali mbaya.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro Basil Lema, amesema Mbowe alianza kuugua gafla wakati akipata chakula cha mchana katika Hoteli ya Keys, Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

“Tulikuwa tukipata chakula cha mchana katika Hoteli ya Keys lakini Mwenyekiti alisema anajisikia vibaya na afya yake haiko sawa hivyo akataka tumpeleke hosptali ya KCMC kwa ajili ya kuangalia afya yake zaidi.

“Baada ya kumfikisha hosptalini hapo madaktari bingwa walimpima afya yake na kumtaka kubaki chini ya uangalizi wa madaktari kwa matibabu zaidi,” amesema.
Na Upendo Mosha- Mtanzania Moshi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post