Friday, March 2, 2018

JINSI MLIPUKO WA TRANSFOMA ULIVYOZUA KIZAA ZAA MAHAKAMANI DAR

  Malunde       Friday, March 2, 2018
Shughuli katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zilisimama kwa muda baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme katika transfoma ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) iliyopo katika eneo la mahakama hiyo.


Trasfoma hiyo imelipuka na kusababisha nyaya mbili kushika moto na kuzua hofu miongoni mwa watu waliokuwa mahakamani hapo, kuanza kukimbia hovyo.


Tukio hilo limetokea asubuhi Machi 1, 2018 wakati kesi mbalimbali zikiendelea kusikilizwa.


Mtendaji wa Mahakama Mkoa wa Dar es Salaam, Gasto Kanyairita amesema baada ya kutokea kwa mlipuko huo ulizuka moto na kushika nyaya mbili, ikiwemo ya intaneti ambazo hutumiwa kwa ajili ya mawasiliano ya simu.


"Moto uliingia moja kwa moja katika jengo letu na kushika seva yetu ambayo tunatumia kwa ajili ya mawasiliano ya simu,” amesema.


"Baada ya kushika nyaya hizo, moto huo uliambaa amba na kuingia katika chumba cha Tehama na kisha kushika soketi ya umeme iliyopo ndani ya jengo la mahakama.”


Baada ya kutokea kwa hitilafu hiyo ya umeme, askari polisi walikuwepo mahakamani hapo, alitumia vidhibiti moto na kufanikiwa kuuzima.


Dakika tano, baada ya kutokea kwa hitilafu hiyo, gari la zimamoto lilifika mahakamani hapo na kukuta tayari moto huo umezimwa.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post