DIAMOND AJILIPUA " SIOGOPI JELA...UNANIFUNGIA NYIMBO ZANGU UMESHAWAHI KUCHANGIA NINI KATIKA MUZIKI WANGU...? | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, March 20, 2018

DIAMOND AJILIPUA " SIOGOPI JELA...UNANIFUNGIA NYIMBO ZANGU UMESHAWAHI KUCHANGIA NINI KATIKA MUZIKI WANGU...?

  Malunde       Tuesday, March 20, 2018
Msanii wa muziki Bongo, Diamond amefunguka kuhusu kufungiwa kwa nyimbo zake mbili ‘Waka na Hallelujah’ kwa kueleza kuwa ni kitu ambacho hakiwezi kumpunguzia chochote na hakiwezi kujenga muziki wa Tanzania.

Muimbaji huyo ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa yupo tayari kupigania muziki wake kwa lolote lile na iwapo kuna sehemu ambayo wao kama wasanii wanaenda kinyume ni jambo la kuelekezana.

“Suala si kufungia tu nyimbo, mimi ukinifungia nyimbo hainipunguzii kitu nikienda nje naenda nai-perform ukiwa hutaki si naondoka tu naenda nchi nyingine, kwa hiyo ni kukaa tuzungumze, tuelekezane lakini tusifanye kama kukomoana, hapana, tufanye katika mazingira ambayo yatasaidia sanaa ikue." Alisema Diamond na kuongeza;

"Huwezi kumfungia mtu kama Roma kwa miezi sita,unajua kuwa anachangamoto gani?umeshawahi kutaka kuzitatua?

"Unanifungia nyimbo zangu umeshawahi kuchangia nini katika muziki wangu , utamnunulia Tiffah wewe pampers?

"Simuogopi mtu hata kama jela mimi nitaenda kwa ajili ya kuukomboa muziki .ntaitetea bongo fleva kwa sababu naijua kuliko anavyoijua yeye anaetufungia , sio unakuja unafungia bila hata kufanya research, anakuja na atatuacha sisi hapa."

Diamond ambaye anaonekana kujiamini kuwa hata iweje lazima atasimama kwa ajili ya bongo fleva, anasema kuwa wala hajali kwa sababu hajapata taarifa rasmi juu ya kufungiwa kwa nyimbo zake zaidi ya kuziona habari katika mitandao ya kijamii.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post