Wednesday, March 21, 2018

DIAMOND AELEZA BIFU YAKE NA ALI KIBA ILIVYOSUKWA ‘KUMUUA KIMUZIKI’

  Malunde       Wednesday, March 21, 2018
Diamond Platinumz amedai kuwa uhasama kati yake na Ali Kiba ulipikwa na chombo kimoja cha habari kwa lengo la kumuondoa kwenye ramani ya muziki.


Bosi huyo wa WCB amefunguka katika mahojiano na Lil Ommy wa Times FM, ambapo amedai kuwa uhasama huo ulikuwa miongoni mwa mbinu za muda mrefu zilizoshindwa za kutaka kumuua kimuziki.


Amesema kuwa baada ya kugundua mbinu hiyo, alikutana na Ali Kiba jijini Nairobi na akazungumza naye kuhusu hilo na wakakubaliana hakuna tofauti kati yao.


Diamond ambaye anapromoti albam yake mpya ya ‘A Boy From Tandale’ alisema kuwa tofauti kati yake na Ali Kiba haiko kiuhalisia kwani inatengenezwa na watu wasiomtakia mema na kukuzwa na mashabiki. 


Aliongeza kuwa njama na jitihada za kutaka kumuangusha kimuziki zilianza miaka minne iliyopita lakini haziwezi kufanikiwa. Alisisitiza kuwa hakuna anayeweza kumuua kimuziki akiwa hai, “labda unitoe uhai, lakini kuniua kimuziki haiwezekani.”


Lil Ommy alitaka kujua kama nyimbo za Ali Kiba zitachezwa kwenye vituo vya Wasafi Radio na Wasafi TV.


“Bro nisikudanganye, pale atachezwa kila msanii na yeyote mwenye talent (kipaji). Hadi sasa pale watu wanabishana kuhusu slogan (kauli mbiu), kuna wanaosema ‘Welcome Home’ na ‘Hii ni Yetu Sote’. Kwa hiyo hii ni ya wasanii na haipo kwasababu ya matabaka,” alijibu.Chibu alisema kuwa ushikirikiano wa wasanii ndio utakaoendelea kuukuza muziki wa Bongo Fleva na sio uhasama na ushindani usiokuwa na lengo zuri.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post