Monday, March 12, 2018

DC AAGIZA POLISI KUMKAMATA MENEJA WA IDARA YA MAJI KWA KUKOSESHA WANANCHI MAJI SIKU TATU

  Malunde       Monday, March 12, 2018
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro, Sirieli Nchembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata Meneja wa Idara ya Maji wa Wilaya hiyo kwa kusababisha ukosefu wa maji kwa siku tatu mfululizo.

Mkuu huyo wa Wlilaya ameseme Meneja anayejulikana kwa jina la Herman Mundo, pamoja na watumishi wa idara hiyo walisababisha uharibifu wa miundo mbinu ya maji na kusababisha kukosekana kwa huduma ya maji safi kwa zaidi ya siku tatu wilayani hapo.

Agizo hilo katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani, kilicholenga kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya alipokea malalamiko toka kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya akidai kumekuwa na mchezo kwa baadhi ya viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia sekta ya maji kwa kuingiza migogoro binafsi katika sekta hiyo hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi ikiwemo kukosekana kwa huduma ya maji.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post