Monday, March 12, 2018

AUA WATOTO WATATU WA MKE MWENZIE KWA MTEGO WA UJI....AJIUA

  Malunde       Monday, March 12, 2018

Mwanamke mmoja katika kijiji cha Nyahera Kaunti ya Kisumu nchini Kenya, amewaua watoto watatu wa mke mwenzie, na kisha mwenyewe kujinyonga.

Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki hii ya tarehe 11, Machi, ambapo limeelezwa kwamba mwanamke huyo anayejulikana kwa jina la Jacinta Otieno, aliwaita watoto hao ambao walikuwa wanne kwenda kunywa uji nyumbani kwake, na ndipo alipoanza kuwacharanga na mapanga mpaka kuwaua na kisha mwenyewe kujinyonga, huku mtoto mmoja akinusurika baada ya kukata kwenda kunywa uji.

Jacinta alifanya tukio hilo baada ya mke mwenzie kwenda kanisani na kuwaacha watoto peke yao nyumbani ambako wanaishi jirani, huku mume wao akiishi jijini Nairobi na watoto wawili ambao amewazaa yeye.

Kwa mujibu wa majirani wawili hao wameelezwa kuwa hawakuwa na maelewano mazuri kutokana na wivu kwa mume wao, na kwamba Jacinta alishajaribu kutaka kujiua wiki moja iliyopita.

Watoto hao waliouawa walikuwa na umri wa miaka 7, 4 na 2, walikuwa wa mke mwenzie Hellen Otieno.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post