ASKARI POLISI AGONGWA GARI BARABARANI AKIONGOZA MAGARI DAR


Askari wa usalama barabarani anayejulikana kwa jina la Sajenti Peter amegongwa na gariwakati akitekeleza majukumu yake ya kusimamia usalama barabarani jijini Dar es Salaam. 

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo imetokea  jana asubuhi majira ya saa 5 katika makutano ya barabara ya Kajenge na Rose Garden eneo la Sayansi ilipokuwa akiongoza magari

Juma Husein ambaye ni mkazi wa Sinza amesema, ajali hiyo imesababishwa na gari aina Hucher maarufu kama Daladala kushindwa kufunga breki baada ya kusimamishwa na trafiki na kisha kuligonga gari dogo aina ya Subaru ambalo lilikuwa limeruhusiwa kuondoka na kusababisha ajali iliyopelekea trafiki huyo kugongwa na gari jingine. 

Ajali hiyo imetajwa kuhusisha magari matatu, majeruhi akiwemo trafiki huyo walikimbizwa hosptali kwa matibabu zaidi, aidha Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa trafiki huyo alivunjika mkono.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.