WAFUASI 28 WA CHADEMA WALIOKAMATWA WAKIANDAMANA DAR WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Watu 28 wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakituhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali na kinyume na sheria.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo mbele ya hakimu mkazi, Godfrey Mwambapa na kusomewa shtaka la kufanya mkusanyiko usiyo halali na Wakili wa serikali, Faraji Nguka


Wakili Faraji Nguka, amedai kosa hilo wamelitenda February 16, 2018 barabara ya Kawawa maeneo ya Kinondoni Mkwajuni ambapo walifanya mkusanyiko usio halali wakiwa na nia ya kusababisha uvunjifu wa amani.

Baada ya kusomewa kosa hilo washtakiwa walikana ambapo Wakili Nguka ameeleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo, Hakimu Mwambapa alitoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa ambapo wametakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini Bondi ya Sh.Milioni 1.5

Washitakiwa hao wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 3, 2018 itakapotajwa.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.