TLS YAMMWAGIA SIFA RAIS MAGUFULI

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Godwin Ngwilimi amepongeza Rais  John Magufuli kwa kutekeleza matarajio ya watanzania.

 Ngwilimi ametoa kauli hiyo leo Februari mosi jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria na uzinduzi wa mwaka mpya wa kimahakama.

Pia, ameomba uwezeshaji wa rasilimali fedha katika muhimili wa mahakama ili kushughulikia changamoto zinazoikabili. "Kama chama cha mawakili, tunakuunga mkono na tunaahidi kutoa ushirikiano kwa mahakama pale inapostahili."

Ametoa wito akisema, watumishi wa mahakama, majaji, wasajili, watendaji , makarani  na watumishi wengine, mawakili, wanasheria popote walipo wanatakiwa  kutambua mwelekeo wa nchi unabadilika kwa kasi, matarajio ya wananchi , kuondokana na utamaduni wa kuendelea kufanya kazi kimazoea, kutumia fursa zilizopo ikiwamo Tehama ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Pia  kuendelea kusimamia maadili ya kitaaluma na uadilifu , hata Mungu anapenda uadilifu na imeandikwa katika vitabu vitakatifu, kulinda na kuhifadhi misingi ya kitaaluma na kujifunza kwa kufuata makosa yaliyotokea hapo nyuma

Ngwilimi ametoa  wito akisema: " Kama sehemu ya watanzania, tusitumie mahakama vibaya, kusumbua wengine, kuonea wengine, kama sehemu ya majaribio, siyo maabara , kama jumba la kamari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527