RAIS MAGUFULI AWATUNUKU KAMISHENI MAOFISA 197 WA JWTZ


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni maofisa wanafunzi 197 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Sherehe hizo zimefanyika leo Februari 3, 2018 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo maofisa hao wapya ni wa Tanzania na kutoka nchi marafiki, waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli mkoani Arusha. 

Katika tukio hilo ambalo lilipambwa na magwaride kutoka kwa Wanajeshi hao, lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa.

Miongoni mwa waliotunukiwa kamisheni hizo wanawake ni 28, na waliobaki ni wanaume.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.