RAIS MAGUFULI ATEUA MNADHIMU MKUU WA JWTZ





Rais John Magufuli amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Taarifa ya Ikulu imesema uteuzi huo umefanyika leo Februari 14,2018.

Pia, amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Mwakibolwa ambaye amestaafu.

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Mohamed ataapishwa kesho Februari 15,2018 saa tano asubuhi, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli pia amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali J.G. Kingu, M.S. Busungu, R.R. Mrangira, B.K. Masanja, G.T. Msongole, A.F. Kapinga, K.P. Njelekela, A.S. Bahati, M.E. Mkingule na S.S. Makona.


Taarifa ya Ikulu imesema mabrigedia jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527