MBUNGE ASEKWA RUMANDE SAA 48 KWA AMRI YA MKUU WA WILAYA


Mbunge wa Tunduma, wilayani Momba mkoani Songwe, Frank Mwakajoka amekamatwa na polisi kisha kuwekwa mahabasu kwa saa 48 kwa kile kinachodaiwa ni amri ya mkuu wa wilaya hiyo, Jumaa Irando.


Akizungumza na gazeti hili leo Februari 21, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Mkoa wa Songwe, Ayub Sikagonamo amesema Mwakajoka amekamatwa akiwa kituo cha polisi Tunduma kuitikia wito wa Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo (OCD) baada ya kumpigia simu kwamba anamhitaji ofisini.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange alisema ‘Nipo nje ya ofisi, in-short’ kisha akakata simu.


Hii ni mara ya pili kwa Mbunge Mwakajoka kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa saa 48 kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya. Agosti mwaka jana Irando aliamuru kukamatwa Mwakajoka kwa kile alichodai alitoa lugha ya kumdhalilisha yeye na Serikali ya Mkoa wa Songwe wakati akiwa kwenye mkutano wa hadhara.


Na Godfrey Kahango, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527