Friday, February 2, 2018

WASHINDI 43 WA BAHATI NASIBU YA V.I.P CLUB INAYOENDESHWA NA BONITE BOTTLERS WAPATIKANA .

  Malunde       Friday, February 2, 2018


Makasha yakiwa na tikei za bahati kutoka kwa Mawakala wa Bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha Vinywaji Baridi cha Bonite Bottlers cha mjini ,kinachoendesha Bahati nasibu kwa wateja wake wakubwa wajulikanao kama V.I.P Club .
Mwandishi wa Habari wa kituo cha radio cha Kili Fm ,Mwanahamisi Jingu akizungusha pipa lenye tiketi za bahati wakati wa droo ya kuwapata washindi iliyofanyika katika kiwanda cha vinywaji Baridi cha Bonite Bottlers Ltd cha mjini Moshi.
Mwandishi wa Habari Robert Minja akizungusha pipa lenye tiketi za bahati wakati wa droo ya kuwapata washindi iliyofanyika katika kiwanda cha vinywaji Baridi cha Bonite Bottlers Ltd cha mjini Moshi.
Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Bonite Bottlers Ltd ya mjini Moshi Christopher Loiruk ,akitaja majina ya washindi katika Droo ya kupata washindi wa Bahati nasibu kwa Wateja wakubwa wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo.


Zawadi za Pikipiki 25 zilizotolewa kwa washind wa Bahati Nasibu kwa wateja wakubwa wa bidhaa za Cocacola zinazozalishwa na Kampuni ya Bonite Bottlers ya Mjini Moshi.
Sanduku 100 na Sanduku 50 pia zilikuwa ni miongoni mwa zawadi ambazo washindi 43 walijinyakulia baada ya kushiriki bahati Nasibu hiyo.
Washiriki wa Bahati Nasibu kwa Wateja wakubwa wa Bidhaa jami ya Cocacola wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya baadhi yao kutangazwa washindi wa Droo iliyofanyika kiwandani hapo.
Washiriki hao walipata pia fursa ya kutembelea maene mbalimbali ya kiwanda hicho kujionea hatua mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa Jamii ya Cocacola.

Uzalishaji wa Cocacola ukiendelea katika kiwanda cha vinywaji baridi cha Bonite Bottlers cha mjini Moshi .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda a Kaskazini .


WASHINDI wa bahati nasibu kwa wateja wakubwa wa Vinywaji baridi vya jamii ya CocaCola wamepatikana baada ya Kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ya mkoani Kilimanjaro
kuchezesha droo ya kwanza ambapo jumla ya washindi 43 wamejinyakulia zawadi.

Miongoni mwa zawadi kubwa ambazo washindi hao wamejinyakulia ni pamoja na Pikipiki 25
,sanduku 100 na sanduku 50 kwa washindi watatu wa mikoa ya mauzo ya bidhaa za CocaCola ya Arusha,Kilimanjaro ,Manyara na Singida .

Christopher Loiruk ni Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ameeleza namna ambavyo washindi hao wamepatikana kuwa ni kwa kununua sanduku tano za Soda zinazozalishwa na kiwanda hicho kasha unajipatia tiketi inayokuingiza katika Droo maalum..

Nao baadhi ya wateja wa vinywaji baridi jamii ya Cocacola vinavyozalishwa na Bonite waliofanikiwa kushinda katika Droo hiyo wameonesha furaha yao huku wakitoa wito
kwa wateja wengine kuendelea kushiriki katika bahati nasibu hizo.

Kabla ya kuchezeshwa kwa Dro hiyo iliyosimamiwa na Mwakilishi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha Humud AbdulHussein wateja wa vinywaji baridi jami ya Cocacola
walipata nafasi ya kutembelea kiwanda cha Bonite na kujionea na kupata maelezo namna ambavyo bidhaa za soda na maji zinavyozalishwa katika kiwanda hicho.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post