KINGUNGE NGOMBALE KUZIKWA JUMATATU MAKABURI YA KINONDONIMwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru anatarajiwa kuzikwa Jumatatu Februari 5, 2018 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa kamati ya maziko ya mwanasiasa huyo, Omary Kimbau amesema Kingunge atazikwa saa tisa alasiri.

Hata hivyo, amesema leo Ijumaa Februari 2,2018 kuwa utaratibu na mipango mingine inaendelea kufanyika.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.