HAKIMU AFARIKI GHAFLA DAR


Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Juma Hassan Kasailo amefariki dunia ghafla jana jioni Februari 23, 2018.

Taarifa za kifo cha hakimu huyo zimethibitishwa na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ilvin Mugeta.

"Mimi niko safarini, lakini ninazo taarifa hizo kuwa Hakimu Kasailo amefariki dunia,” amesema Mugeta leo Jumamosi Februari 24 alipozungumza na MCL Digital.

Kasailo atazikwa kesho Jumapili Februari 25, saa 7:30 mchana Segera kwa Msisi, wilayani Korogwe mkoani Tanga. 

Mwili wa marehemu unaagwa leo mchana nyumbani kwake, Chanika Buyuni jijini Dar es Salaam.

Na Magai Magai, Mwananchi 
Theme images by rion819. Powered by Blogger.