DMF, MAKJUICE WAWAPA FARAJA WAZAZI WA WATOTO NJITI HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR KATIKA SIKU YA WAPENDANAO


Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel (wa tatu kulia) akimkabidhi mmoja wa wauguzi wa zamu wa Wodi ya Watoto Njiti katika Hospitali ya Mwananyamala, sehemu ya msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati katika Hospitali hiyo ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya kuonyeshana upendo (Valentine's Day) ambayo huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Februari 14. 

Taasisi ya Doris Mollel walishirikiana na Kampuni ya MakJuice na baadhi ya wapigapicha, wanahabari pomoja na wadau wengine waliojitoa kufanikisha zoezi hilo, lililofanyika jana jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Warda Walid (Muwakilishi wa Taasisi ya DMF Zanzibar), Mariam Gerion (DMF Dar es salaam), Mtangazaji wa Clouds TV, Shadee pamoja na baadhi ya wauguzi wa Hospitali hiyo.
Picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada huo pamoja na vitu vingine mbalimbali.
Mwakilishi wa wa Kampuni ya MakJuice, Zahir akimkabidhi zawadi ya khanga mmoja wa akina mama waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel akizungumza jambo na mmoja wa kinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Akina mama waliojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), wakipoza koo zao na Juice za Mak walipotembelea Hospitalini hapo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527