CHELSEA YAFUFUKIA DARAJANI, YAICHAPA WBA 3-0


Magoli mawili ya kiungo Eden Hazard na moja la Victor Mosses yameipa Chelsea ushindi wa 3-0 dhidi ya West Bromwich Albion usiku wa kuamkia leo Jumanne Februari 13,2018.

Kwa ushindi huo, The Blues wamepanda hadi nafasi ya nne ya Ligi Kuu ya England na kuzidi kuididizima West Bromwich Albion katika nafasi za chini ya msimamo huo.

Wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani, Stanford Bridge, The Blues wameweza kufuta kumbukumbu mbaya waliyoipata wiki iliyopita baada ya kuchabangwa 4-1 na Watford.

Manchester City bado ni kinara wa ligi hiyo, wakifuatiwa kwa mbali na majirani wao, Manchester United na Liverpool. Tottenham ipo nafasi ya sita ya msimamo huo huku Arsenal ikiwa imetupwa hadi nafasi ya sita ya msimamo huo.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.