Sunday, March 4, 2018

FILAMU YA 'LAANA YA MKE' KUZINDULIWA MACHI 23 ..TAZAMA TRAILER HAPA

  Malunde       Sunday, March 4, 2018

Mwaka mmoja baada ya kuachia Filamu ya ‘Nyama ya Ulimi’,Bongo Movies Shinyanga wanakuletea Filamu nyingine kali inaitwa “Laana ya Mke” ambayo itazinduliwa rasmi Machi 23,2018.

Filamu hiyo yenye ubora wa hali ya juu inahusu majanga na laana wanazopata wanaume wababe,wasio na fadhila wanaotafuta mali na wake zao kisha kuwafanyia ukatili.

Katika Filamu hii iliyoongozwa na Director mahiri Dave Skerah wamo Magwiji wa Filamu akiwemo Blandina Chagula ‘Johari’, Ibrahim Songoro ‘Songoro Gadafi’,Magreth Emmanuel, Mariam Bilal, Najma Shahel,Edward Joseph na Mzee Salum Kawelewele.

Mwenyekiti wa Bongo Movies Shinyanga Juma Ibrahim Songoro ameiambia Malunde1 blog kuwa uzinduzi wa filamu ya Laana ya Mke utafanyika tarehe 23.03.2018 katika ukumbi wa NSSF ya zamani “CCM mkoa wa Shinyanga” kuanzia saa tatu usiku.

TUMIA DAKIKA ZAKO 2 TU KUANGALIA KIONJO CHA FILAMU YA LAANA YA MKE
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post